JPM kuhutubia mkutano wa hadhara Jumapili

Muktasari:

Rais John Magufuli anatarajia kufanya ziara wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambako atafanya mkutano wa hadhara kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Kahama. Rais John Magufuli anatarajia kufanya ziara wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambako atafanya mkutano wa hadhara kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu alisema jana kwamba Rais Magufuli atawasili Kahama Jumamosi jioni kabla ya kufanya mkutano wa hadhara Jumapili.

Nkulu aliwataka wananchi wa Kahama na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kumlaki kiongozi huyo katika ziara hiyo ambayo alisema: “Lengo lake ni kuwapongeza wananchi wa Kahama kwa kumpa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika mwaka jana.”