JWTZ yajifua dhidi ya ugaidi

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakionyesha utayari wakati wa uzinduzi wa mazoezi ya kijeshi ya pamoja yaliyofanyika kwenye Kambi ya Wanamaji Kigamboni jijini Dar es Salaam juzi, ikiwa ni maadhimisho ya miaka 52 ya jeshi hilo. Picha na Said Khamis

Muktasari:

  • Jeshi hilo limesema linajiimarisha kwa mazoezi na mafunzo ili liwe na uwezo wa kukabiliana na viashiria vya ugaidi.

Dar es Salaam. Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limejipanga kukabiliana na vitendo vya ugaidi nchini. 

Jeshi hilo limesema linajiimarisha kwa mazoezi na mafunzo ili liwe na uwezo wa kukabiliana na viashiria vya ugaidi.

Akizungumza wakati akifungua mazoezi ya pamoja ya kijeshi ambayo yamehusisha kamandi  za kikosi cha anga, maji na vikosi vya akiba vya mgambo, Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Venance Mabeyo amesema Tanzania kama ilivyo kwa nchi jirani ina viashiria vya ugaidi ambavyo havitaachwa vikue na kuota mizizi.

Amesema nchi jirani zimekuwa zikikabiliana na matukio ya ugaidi na hapa nchini kuna viashiria vinavyoonyesha kuwapo watu wa aina hiyo.