Rais Magufuli ateua mnadhimu mkuu wa JWTZ

Muktasari:

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Mohamed ataapishwa kesho Februari 15,2018.  


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Meja Jenerali Yakubu Hassan Mohamed kuwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Taarifa ya Ikulu imesema uteuzi huo umefanyika leo Februari 14,2018.

Pia, amempandisha cheo kutoka Meja Jenerali na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali  Mohamed anachukua nafasi ya Luteni Jenerali James Mwakibolwa ambaye amestaafu.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Mohamed ataapishwa kesho Februari 15,2018 saa tano asubuhi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli pia amewapandisha vyeo kutoka Brigedia Jenerali na kuwa Meja Jenerali J.G. Kingu, M.S. Busungu, R.R. Mrangira, B.K. Masanja, G.T. Msongole, A.F. Kapinga, K.P. Njelekela, A.S. Bahati, M.E. Mkingule na S.S. Makona.

Taarifa ya Ikulu imesema mabrigedia jenerali wote waliopandishwa vyeo watapangiwa vituo vya kazi baadaye.