Jafo aahidi makubwa Serengeti

File Photo

Muktasari:

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jafo amesema kupitia makusanyo ya kodi na kubana matumizi, Serikali itahakikisha huduma hizo zinaboreshwa kwa kuwa wilaya hiyo ni kitovu cha utalii.

Serengeti. Serikali imepanga kuboresha barabara, huduma za afya na maji kwa wakazi wa Serengeti mkoani Mara.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Suleiman Jafo amesema kupitia makusanyo ya kodi na kubana matumizi, Serikali itahakikisha huduma hizo zinaboreshwa kwa kuwa wilaya hiyo ni kitovu cha utalii.

Amesema Serikali imejielekeza katika kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo ili kuharakisha kukuza uchumi.