Jenerali Ulimwengu apata ajali, alazwa MOI

Jenerali Ulimwengu

Muktasari:

Akizungumza na Mwananchi, Ofisa Uhusiano wa MOI Patrick Mvungi alisema wamempokea Ulimwengu akiwa ametokea katika kitengo cha dharura hospitali ya taifa Muhimbili na kumfanyia vipimo mbalimbali mchana wa leo.

Dar es Salaam. Mwanaharakati ambaye pia ni mwandishi mkongwe, Jenerali Ulimwengu amelazwa katika Taasisi ya Upasuaji wa Mifupa (MOI), baada ya kuokotwa na wasamaria wema eneo la ubalozi wa Ufaransa, Masaki, usiku wa kuamkia leo akiwa hajitambui baada ya kupata ajali ya gari.

Akizungumza na Mwananchi, Ofisa Uhusiano wa MOI Patrick Mvungi alisema wamempokea Ulimwengu akiwa ametokea katika kitengo cha dharura hospitali ya taifa Muhimbili na kumfanyia vipimo mbalimbali mchana wa leo.

“Tumempokea akitokea kitengo cha dharura Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) hapa kwetu amekuja kwa dharura, tumefanikiwa kumfanyia vipimo kadhaa na sasa amelazwa wodini. Tatizo kubwa alilolipata ni kuumia kichwani,” alisema Mvungi.