Jinsi polisi wanne walivyouawa kinyama Dar

Muktasari:

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani askari walioshambuliwa na kupoteza maisha ni E.5761CPL Yahaya (dereva), F.4660 CPL Hatibu, G.9524 PC Tito na G.9996 PC Gastone.

Dar es Salaam. Ilikuwa kama mtu anaangalia sinema.  Watu tisa waliokuwa kwenye pikipiki tatu walijitokeza ghafla katika Benki ya CRDB tawi la Mbande, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam na kulimiminia risasi gari la polisi lililokuwa ndiyo kwanza linawasili katika eneo hilo kuleta askari kwa ajili ya lindo la usiku. Askari watatu walikufa palepale na mmoja alifia njiani wakati akipelekwa hospitali.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Marijani askari walioshambuliwa na kupoteza maisha ni E.5761CPL Yahaya (dereva), F.4660 CPL Hatibu, G.9524 PC Tito na G.9996 PC Gastone.

Kamishna Marijani alisema katika tukio hilo wakazi wawili wa Mbande, Ally Chiponda na Azizi Yahaya walijeruhiwa.

“Majambazi hao hawakuiba chochote wala kuharibu mali yoyote katika benki ile na mara baada ya mauaji hayo waliondoka na bunduki mbili aina ya SMG zikiwa na risasi 60,” alisema Kamishana Marijani.

Habari zaidi soma Gazeti la Mwananchi