Johari azungumzia ndoa ya Uwoya na Dogo Janja

Muktasari:

Johari ni kati ya wasanii wachache waliobahatika kualikwa kwenye harusi hiyo ambapo inaelezwa alisimama kama ndugu upande wa mwanamke.


Msanii Blandina Chagula maarufu Johari anayeelezwa kuwa mtu wa karibu wa Irene Uwoya, amesema mpaka sasa kama kuna mtu anadhani ndoa ya Uwoya na msanii wa bongo fleva, Dogo Janja ilikuwa ni maigizo wasubiri kuletewa CD.

Akizungumza na MCL Digital leo Machi 24, amesema anachojua ni kwamba wawili hao wamefunga ndoa ya ukweli na kwa wale ambao hawaamini hawezi kuwalazimisha.

Johari ni kati ya wasanii wachache waliobahatika kualikwa kwenye harusi hiyo ambapo inaelezwa alisimama kama ndugu upande wa mwanamke.

Hata hivyo, kitendo hicho kimeonekana kumkera mama wa Uwoya, Naima Mrisho, ambaye amesema ndoa hiyo wao hawaitambui na kutaka waulizwe watu waliojiita ni ndugu wa Uwoya waliosimamia shughuli hiyo akiwemo Johari na kiongozi wa dini aliowafiungisha.

Alipoulizwa ni kwa nini hakumuuliza rafiki yake huyo walipo wazazi siku ya ndoa, Johari alijitetea kwamba ingekuwa ngumu ukizingatia kwamba alipata mualiko saa chache kabla ya harusi na insingekuwa rahisi kukaa na kumuuliza Uwoya.

“Jamani pia ieleweke Uwoya na Dogo Janja ni watu wazima, wana maamuzi yao ambayo hayapaswi kuingilia na kama ni kupendana wamependana wenyewe,” amesema na kuongeza:

“Suala la kuanza kuwauliza maswali mengi juu ya namna walivyoifanya harusi yao bila uwepo wa wazazi sio sahihi kwani walijua wanachokifanya.”

Oktoba 28, mwaka jana, Uwoya na Dogo Janja walifunga ndoa ya kimyakimya ambayo ilizua gumzo kutokana na kuwepo kwa tofauti kubwa ya umri kati yao na hadi leo familia ya Uwoya imekataa kuitambua ndoa hiyo.Your "Inbox" folder is empty

Settings