Kabila kuhutubia bunge leo

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila.

Muktasari:

Nchi hiyo kubwa barani Afrika ipo katika taharuki ya ikiwa Kabila atagombea katika uchaguzi ulioahirishwa kwa muda mrefu ukiwa umepangwa kufanyika  Desemba licha ya muhula wake kikatiba kumalizika mwaka 2016.

DRC. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila anatarajiwa kulihutubia bunge hii leo, ikiwa ni chini ya wiki moja kabla ya wagombea hawajaanza kujisajili kwa ajili ya uchaguzi wa rais.

Nchi hiyo kubwa barani Afrika ipo katika taharuki ya ikiwa Kabila atagombea katika uchaguzi ulioahirishwa kwa muda mrefu ukiwa umepangwa kufanyika  Desemba licha ya muhula wake kikatiba kumalizika mwaka 2016.

 Rais Kabila amekataa kutangaza hadharani iwapo atagombea muhula mwingine madarakani au la, na wagombea urais wanatarajiwa kujisajili kati ya Julai 25,na Agosti Mosi.

 Wiki iliyopita katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema alikubali kuahirisha ziara yake nchini DRC ili kumruhusu Kabila kutangaza uamuzi mzito.

Kabila ambaye alichukua madaraka kutoka kwa baba yake aliyeuawa 2001, alimaliza muhula wake kisheria mwaka 2016 lakini vifungu vya katiba vilimruhusu kuendelea  kubaki madarakani hadi mrithi wake atakapopatikana.