Kafumu, Kamata wajiuzulu uongozi kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Viwanda na Biashara Dk Dalali Kafumu na makamu wa kamati hiyo Vick Kamata, kwa pamoja wamejiuzulu nafasi zao.

Viongozi hao wameeleza sababu za kuchukua hatua hiyo kuwa ni  serikali kuingilia majukumu yao katika utendaji kazi na hivyo wakaeleza kuwa hawaoni sababu za kuendelea na majukumu hayo.

Wamekabidhi barua za kujiuzulu kwenye  ofisi ya spika wa bunge jana.