Kaimu Jaji Mkuu kuapishwa leo jioni

 Rais John  Magufuli, anatarajia kumuapisha Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma leo (Jumatano) saa 10.00 jioni.

Muktasari:

  • Tukio la kuapishwa kwa Profesa Juma litarushwa moja kwa moja na vituo vya redio na televisheni vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

Dar es Salaam. Rais John  Magufuli, anatarajia kumuapisha Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma leo (Jumatano) saa 10.00 jioni.

Tukio la kuapishwa kwa Profesa Juma litarushwa moja kwa moja na vituo vya redio na televisheni vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), na tovuti rasmi ya Ikulu ambayo ni www.ikulu.go.tz

Profesa Juma aliteuliwa jana kushika nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mkuu, Mohamed Chande aliyestaafu.

Kabla ya kuteuliwa katika nafasi hiyo, Profesa Juma alikuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa nchini.