Monday, July 17, 2017

Kairuki: Ubungo itapata watumishi wapya 397

 

By Cledo Michael, Mwananchi; mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki

amesema kuwa kati ya ajira mpya 15,000 zilizotangazwa, wilaya ya Ubungo itapata watumishi wapya 397.

 

Pia, watumishi 193,166 wanatarajia kupandishwa vyeo kwa mwaka huu.

 

Akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo, leo, Julai 17, Waziri Kairuki amesema wizara imeboresha mifumo ya Tehama ili kudhibiti vyeti feki na udanganyifu.

 

"Lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunakuwa na taarifa sahihi za watumishi wa umma, lakini pia ni kuunganisha mifumo yetu ya kimkakati ya Tehama ya Serikali ili iweze kuzungumza,” amesema.

 

Amewataka kuhakikisha taarifa za baraza la mitihani, uhamiaji, TRA, Rita, ziweze kufanana na mfumo wa kielektroniki wa malipo (Lawson).

 

Amewataka watumishi wa umma kuendelea kuhakiki taarifa zao hasa za vyeti vya taaluma kwa kuwa zoezi hilo ni la kudumu.  

-->