Kamati ya Bunge yabaini dosari usambazaji wa dawa

Muktasari:

Wizara ya Afya imeomba Sh886 bilioni kwa mwaka 2018/19, lakini iliomba Sh1.07trilioni kwa 2017/28.

 


Dodoma. Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii imesema licha ya usambazaji wa dawa muhimu kuongezeka kwa asilimia 89.6, bado kuna changamoto ya dawa hizo kumfikia mgonjwa na kuitaka Serikali kuchunguza chanzo cha kuchelewa kwa dawa hizo.

Akiwasilisha maoni ya kamati kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2018/19, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba amesema: “Bado kumekuwa na changamoto ya dawa hizo kumfikia mlaji kwa maana ya mgonjwa anapokwenda katika kituo cha kupata huduma ya afya.”

“Serikali ifanye utafiti mdogo wa kuona dawa hizi zinaishia wapi licha ya usambazaji kuongezeka kwa asilimia kubwa ili kuweza kuitatua changamoto hiyo. Hitaji la mgonjwa mmoja mmoja ni kupata dawa pale anapohitaji kutibu ugonjwa unaomsumbua.”