Kambi ya upinzani yadai bajeti yao imekataliwa

Muktasari:

Kwa kawaida, kabla ya kuanza kwa kikao hicho, Msemaji wa Upinzani na Mwenyekiti wa Kamati ya kisekta huwasilisha mezani taarifa zao.


Dodoma. Bajeti mbadala ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliyopangwa kusomwa leo Juni 18, 2018 haitasomwa.

Akizungumza na MCL Digital leo Juni 18, Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Halima Mdee (Chadema) amesema, ofisi ya bunge imekataa kuipokea bajeti ya upinzani iliyowasilishwa jana Juni 17, na badala yake wakasema ipelekwe leo asubuhi, lakini ilipopelekwa pia ikakataliwa.

Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za leo katika Kikao cha 52 cha Bunge la 11 la Bajeti, hotuba ya bajeti ya upinzani haipo katika ratiba.

Kwa kawaida, kabla ya kuanza kwa kikao hicho, Msemaji wa Upinzani na Mwenyekiti wa Kamati ya kisekta huwasilisha mezani taarifa zao.

Lakini leo, kilichofanyika ni  Spika wa Bunge, Job Ndugai kumwita Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Hawa Ghasia ambaye aliwasilisha taarifa yake lakini upinzani hawakuiwasilisha na kwa maana hiyo,  hawataisoma.

Juhudi za kuupata uongozi wa bunge, zinaendelea.