Kampuni ya bia yanufaisha wakulima 30,000 nchini

Muktasari:

  • Meneja Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga alisema wanaamini kilimo ni uti wa mgongo katika kuinua uchumi wa nchi

 Ikiwa kesho ni Sikukuu ya wakulima, maarufu kwa jina la Nanenane, Kampuni ya TBL Group imesema mpango wake wa kuendeleza kilimo umewafikia wakulima 30,000 wa mikoa ya kaskazini na Dodoma.

Meneja Mawasiliano wa TBL Group, Zena Tenga alisema wanaamini kilimo ni uti wa mgongo katika kuinua uchumi wa nchi.

Pia, alisema kilimo kinakuza sekta ya viwanda hususan vinavyotengeneza vinywaji kwa kuwa asilimia kubwa vinatumia malighafi za mazao.

“Miaka michache iliyopita, tuliwekeza kuwainua wakulima wa shairi kwenye mikoa ya kaskazini mwa Tanzania na wa zabibu mkoani Dodoma.

Nafurahi kutangaza mpango huu shirikishi tangu uanzishwe na umenufaisha wakulima zaidi ya 30,000 na wananchi wengine 300,000 kwa njia mbalimbali,” alisema.

TBL Group ni kampuni tanzu ya Anheuser-Busch InBev (AB InBev) yenye makao yake makuu nchini Ubelgiji.Alisema kupitia sera yake ya ‘Kujenga Dunia Maridhawa’ kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na wakulima wa shairi na zabibu kuwawezesha kwa njia mbalimbali.