Kampuni za chini zashtuliwa

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai.

Muktasari:

  • Pia, kampuni hizo zimeshauriwa kushiriki tuzo ya kampuni bora 100 za kiwango cha kati, ili kujulikana ndani na nje ya nchi.
  • Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai alitoa wito huo katika uzinduzi wa tuzo hiyo mkoani Arusha jana.

Arusha. Kampuni za daraja la kati na la chini, zimeshauriwa kuchangamkia fursa ya uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kwenda sambamba na mpango wa Serikali ya awamu tano wa kufufua viwanda.

 Pia, kampuni hizo zimeshauriwa kushiriki tuzo ya kampuni bora 100 za kiwango cha kati, ili kujulikana ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai alitoa wito huo katika uzinduzi wa tuzo hiyo mkoani Arusha jana.

Awali, Meneja Mwandamizi ya Kampuni ya KPMG ambao ni waandaaji wenza wa tuzo 100 bora za daraja la kati, Amour Saleh alisema tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo, washiriki wamepata faida katika kuendeleza biashara zao.