Wednesday, June 13, 2018

VIDEO: Katibu Mkuu CCM aanza kutema checheKatibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally 

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally  

By Nazael Mkiramweni, Mwananchi

Dodoma.  Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amesema atawafukuza uanachama watendaji wote watakaoonekana wanabeba mikoba ya wagombea na kushabikia makundi ya siasa ndani ya chama hicho.

Dk Bashiru ameyasema hayo leo Juni 13 akiwa katika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma wakati akizungumza na wanachama pamoja na watumishi wa chama hicho mkoani hapa.

Amesema ni marufuku watendaji wa chama hicho kuwa na makundi ya siasa ndani kwani hali hiyo ikitokea chama hakiwezi kuendelea mbele.

“Ni marufuku mtendaji wa chama kumshangilia mgombea wa kisiasa, kwani hiyo inapelekea kuwa na makundi, sasa tujiulize kila mtendaji akiwa na mgombea wake chama kitakalika?

“Hivyo nitawafukuza watendaji wote ambao wataonekana wanabeba mikoba wa wagombea, waacheni wanachama wa kawaida wafanye hivyo ila si ninyi watendaji ambao mnalipwa hela za wananchama,” amesema.

 


-->