Mahakama yaidhinisha ushindi wa Kenyatta

Muktasari:

Mahakama ya Juu yatupa kesi mbili zilizofunguliwa ikisema hazina msingi.

Nairobi, Kenya. Mahakama ya Juu ya Kenya imethibitisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa marudio wa urais uliofanyika Oktoba 26,2017.

Uamuzi huo wa Mahakama unatoa nafasi kwa kiongozi huyo kuapishwa, hivyo kuanza muhula wa pili wa uongozi wake.

Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga ametupilia mbali pingamizi zilizotolewa na walalamika kwamba kulikuwa na kasoro katika uchaguzi wa marudio kuhusu majina ya wagombea.

Uchaguzi huo uliosusiwa na mgombea wa Muungano wa Nasa, Raila Odinga ulifanyika baada ya matokeo ya uchaguzi wa awali wa Agosti 8,2017 kufutwa na Mahakama kutokana na ukiukwaji wa kanuni na utaratibu.

Akisoma uamuzi leo Jumatatu Novemba 20,2017 Jaji Maraga amesema majaji kwa kauli moja wameamua kwamba kesi zote mbili hazina msingi.

Walalamikaji katika kesi hizo ni Harun Mwau na wanaharakati wawili Njonjo Mue na Khelef Khalif.