Kenyatta atia saini muswada uliozua tafrani bungeni

Muktasari:

Hatua ya Kenyatta kutia saini muswada huo kuwa sheria, ina maana Wakenya hawana budi ila kugharamia ushuru uliopendekezwa kwa bidhaa za petroli, na mapendekezo mengine.

Muswada huo ni uliokuwa amebeba mapendekezo ya Rais ya punguzo la Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika bidhaa ya mafuta kutoka asilimia 16 iliyokuwa imependekezwa awali hadi asilimia nane.

Kenyatta aliurejesha bungeni muswada uliokuwa na mapendekezo ya asilimia 16 akitaka ufanyiwe marekebisho ambapo alishusha VAT hiyo kutoka hadi nane. Wabunge walikuwa wanataka utekelezwaji wake uahirishwe.

Mapendekezo mengine ni utozaji ushuru huduma za usambazaji wa pesa kwa njia ya simu, intaneti, mitandao, na huduma za benki. Rais pia alipendekeza kupunguzwa gharama ya matumizi kwa viongozi wakuu serikalini.

Nairobi, Kenya. Rais Uhuru Kenyatta ametia saini muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2018, ambao ulipitishwa na Bunge Alhamisi katika mkutano uliotawaliwa na mjadala wenye vurumai.
Katika ujumbe wa twita Ijumaa, Kenyatta, ambaye aliwapiga wabunge wa chama cha Jubilee kuwahamasisha muswada huo unaoongeza gharama za maisha upitishwa, aliahidi kuhakikisha anasimamia matumizi sahihi ya fedha za umma.
"Ninatoa ahadi yangu kwamba nitahakikisha matumizi sahihi ya rasilimali za umma kwa ajili ya Kenya bora. Siwezi kurudi nyuma katika vita dhidi ya rushwa," alisema.
Hatua ya Kenyatta kutia saini muswada huo kuwa sheria, ina maana Wakenya hawana budi ila kugharamia ushuru uliopendekezwa kwa bidhaa za petroli, na mapendekezo mengine.
Muswada huo ni uliokuwa amebeba mapendekezo ya Rais ya punguzo la Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika bidhaa ya mafuta kutoka asilimia 16 iliyokuwa imependekezwa awali hadi asilimia nane.
Kenyatta aliurejesha bungeni muswada uliokuwa na mapendekezo ya asilimia 16 akitaka ufanyiwe marekebisho ambapo alishusha VAT hiyo kutoka hadi nane. Wabunge walikuwa wanataka utekelezwaji wake uahirishwe.
Mapendekezo mengine ni utozaji ushuru huduma za usambazaji wa pesa kwa njia ya simu, intaneti, mitandao, na huduma za benki. Rais pia alipendekeza kupunguzwa gharama ya matumizi kwa viongozi wakuu serikalini.
Baada ya mjadala mkali, shughuli ya upigaji kura kuupitisha au kuuondoa ilizua tafrani na hasa baada ya kukosekana kura za kutosha kwa wabunge waliotaka kuuangusha. Ni wabunge 215 pekee waliojitokeza katika kikao cha bunge kilichoongozwa na Spika wa Bunge Justin Muturi.
Baadhi ya wabunge waliopinga mapendekezo hayo walimnyooshea kidole cha lawama Spika Muturi, kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale, kiongozi wa wachache John Mbadi na viongozi wa kamati mbalimbali bungeni, wakiwatuhumu kwamba walishawishi wabunge wasihudhurie kikao hicho ili wasifikie akidi ya theluthi mbili, sawa na wabunge 233 wenye uwezo kisheria kuuzima muswada.
Duale, kwa upande wake alisema ni wajibu wake kuhakikisha mikakati ya serikali imefikiwa. "Lilikuwa jukumu langu kama kiongozi wa wengi bungeni kuhakikisha wanaopinga pendekezo la Rais hawafiki 233. Mimi ni mtetezi wa serikali," alisema.
Vilevile, wabunge walitishia kumwondoa Spika Muturi wakidai hakutenda sawa. Baadaye walitangaza kuwa wataelekea katika mahakama ya juu zaidi ili kupinga mapendekezo hayo.