Kesi mahakama za mafisadi chapuchapu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki

Muktasari:

Akizungumza wakati wa kikao kati ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa mjini hapa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki amesema Jaji Mkuu ameshamaliza kuandaa kanuni na majaji wameshapewa mafunzo.

Dodoma. Mafunzo ya majaji katika kuendesha Mahakama ya Mafisadi yakiwamo ya kanuni za uendeshaji yamekamilika, huku muda wa kusikiliza na kukamilisha mashauri ukiwa usiozidi miezi tisa.

Akizungumza wakati wa kikao kati ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa mjini hapa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utumishi na Utawala Bora), Angella Kairuki amesema Jaji Mkuu ameshamaliza kuandaa kanuni na majaji wameshapewa mafunzo.

Kairuki amesema sekta ya Serikali za Mitaa inaongoza kwa kuwa na majalada mengi ya uchunguzi yanayohusu tuhuma za rushwa na kati ya majalada 3,082 yanayoendelea na uchunguzi, 1,357 sawa na asilimia 44 yanazihusu Mamlaka za Serikali za Mitaa.