Kesi ya Bulaya kuendelea kusikilizwa leo

Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya

Muktasari:

 

Awali kesi hiyo ilifunguliwa Julai 19, 2015 katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza lakini ilitupwa kutokana na uhalali wa wapeleka maombi

Mwanza. Kesi ya kupinga matokeo ya ushindi inayomkabili Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya itaendelea kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza baada ya kuahirishwa wiki iliyopita na Jaji Lameck Mulacha.

 Awali, Wakili anayetetea walalamikaji katika kesi hiyo, Constantine Mtalemwa aliiomba Mahakama kutupilia mbali maombi ya mjibu maombi yaliyotolewa kwa sababu vifungu walivyowasilisha wakati wa kufungua kesi vilikidhi matakwa ya kisheria.

 Kesi hiyo ilifunguliwa Julai 22 baada ya Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam kujiridhisha na upande wa wapeleka maombi.