Kesi ya kumpinga Bulaya sasa kuendelea

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya 

Muktasari:

Mahakama hiyo imeeleza kuwa kesi hiyo itapangiwa tarehe ya kuendelea kusikilizwa chini ya Jaji Mohamed Gwae aliyeanza nayo. 

Mwanza. Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, imeamua kesi ya kupinga ushindi wa Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya na wenzake wawili iendelee kusikilizwa na jaji aliyeanza kuisikiliza awali ili kuendelea na hoja zilizobaki.

Mahakama hiyo imeeleza kuwa kesi hiyo itapangiwa tarehe ya kuendelea kusikilizwa chini ya Jaji Mohamed Gwae aliyeanza nayo.

Akitoa uamuzi huo jana, Jaji Lameck Mulacha amesema katika maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo baada ya Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam kuyatolea uamuzi, yalikuwa na mambo makuu matatu ambayo ni uchaguzi kutokuwa huru na haki, kugubikwa na rushwa na idadi ya wapiga kura kuongezeka kwenye vituo.

Kesi hiyo iliwasilishwa na wananchi wanne ambao ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila.