Kesi ya mtoto wa nyani kutolewa uamuzi

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala imepanga, Mei 31 mwaka huu kutoa uamuzi dhidi ya mshtakiwa Baraka Joshua(23) kama ana kesi ya kujibu au la.

Hatua hiyo imefikia baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi dhidi ya mshtakiwa huyo.

Joshua  maarufu kama mtoto wa nyani, aliishi na nyani baada ya kuzaliwa na kutupwa  porini takribani miaka nane iliyopita katika pori lililopo mkoani Shinyanga, anakabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 9, ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Msingi Kimanga.

Hakimu Catherine Kiyoja anayesikiliza kesi hiyo alipanga  Mei 31, mwaka huu kutoa uamuzi kama mshtakiwa ana kesi ya kujibu au laa.