Kesi ya ubakaji mtoto yapigwa kalenda

Muktasari:

Hali hiyo imetokana na upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imeahirisha kesi ya ubakaji wa mtoto wa miaka sita inayomkabili mkazi wa Manzese, Hussein Mtoro (20) hadi Machi 27.

Hali hiyo imetokana na upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali, Grace Lwila alidai kuwa Januari 20, 2017 mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo katika eneo la Manzese Midizini.

Wakili huyo wa Serikali alidai kuwa mshtakiwa alifanya kosa hilo wakati akijua kosa hilo la jinai na lipo kinyume na sheria.