Kesi za kodi zakwamisha mapato ya Sh2.2 trilioni

File Photo

Muktasari:

Akizungumza katika uzinduzi wa toleo jipya la Ripoti ya Sheria ya Kodi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema jana kuwa malalamiko mbalimbali ya kodi yaliyowasilishwa katika Baraza la Rufani za Kodi husababisha ukusanyaji mapato hayo kusitishwa.

Dar es Salaam. Serikali imesema ucheleweshwaji wa   kesi za kodi umesababisha kukosa mapato ya zaidi ya Sh2.2 trilioni kwa mwaka huu pekee.

Akizungumza katika uzinduzi wa toleo jipya la Ripoti ya Sheria ya Kodi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema jana kuwa malalamiko mbalimbali ya kodi yaliyowasilishwa katika Baraza la Rufani za Kodi husababisha ukusanyaji mapato hayo kusitishwa.

“Fedha hizo zinapotea kwa sababu watu wanapolalamika, kodi hizo zinasitishwa kuendelea kukusanywa hadi kesi zitakaposhughulikiwa,” amesema Dk Kijaji.

Amesema kutoshughulikiwa kwa wakati kesi za kodi na

kuchelewesha haki za walalamikaji kunaikosesha Serikali mapato.