Khatibu: Narudi nyumbani kuandika vitabu

Katibu mstaafu wa Idara ya oganization ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mohamed Seif Khatibu

Muktasari:

Tukio hilo la makabidhiano ya ofisi linafanyika ikiwa ni utekelezaji wa mabadiliko yaliyofanywa katika sekretarieti mwezi huu na Mwenyekiti wa Chama hicho, John Magufuli kupitia vikao vya chama vilivyofanyika Mkoani Didoma.

Dar es Salaam. Katibu mstaafu wa Idara ya oganaizasheni ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Mohamed Seif Khatibu leo amekabidhi rasmi ofisi kwa Katibu mpya wa Idara hiyo, Pereirra Silima huku akieleza mwelekeo wake kwa sasa ni kurudi nyumbani kuendelea na uandishi wa vitabu. 

Tukio hilo la makabidhiano ya ofisi linafanyika ikiwa ni utekelezaji wa mabadiliko yaliyofanywa katika sekretarieti mwezi huu na Mwenyekiti wa Chama hicho, John Magufuli kupitia vikao vya chama vilivyofanyika Mkoani Didoma.

Kwa mujibu wa CCM, Idara hiyo ndiyo inasimamia na kuratibu chaguzi zote za ndani ya chama na za kitaifa ikiwamo uchaguzi wa viongozi, Jumuiya za vyama, Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

"Nimefanya kazi ya kutumikia chama tangu 1978 nikiwa Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa vijana, kwa sasa narudi nyumbani tu, nitaendelea kuandika vitabu," alisema Seif Khatibu ambaye ameandika vitabu kadhaa vya kiswahili vinavyotumika mashuleni kufundishia. 

Nafasi hiyo huongozwa kwa miaka mitano baada ya uteuzi wa Mwenyekiti wa chama kwa kutumikia vigezo vyake anavyoona vinashawishi. Mwaka 2012, Seif Khatibu alikabidhiwa ofisi hiyo na

Asha Abdullah na leo amekabidhi baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitano. 

Kwa upande wake, Silima alimwomba kuendelea kutoa ushirikiano pale atakapohitajika katika ofisi hiyo.