Kiama cha viroba kesho

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba

Muktasari:

"Ili kuharakisha mchakato huu, nadhani sheria za mazingira tutakazotumia zitakuwa na nguvu zaidi,”alisema Makamba kwa simu leo.

Dar es Salaam. Jeuri ya watumiaji na wazalishaji pombe maarufu viroba, huenda kesho ikapatiwa dawa baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba kueleza utaratibu utakaotumika kuondoa sokoni matumizi ya pakiti za plastiki za kufungushia pombe hizo.

“Ili kuharakisha mchakato huu, nadhani sheria za mazingira tutakazotumia zitakuwa na nguvu zaidi,”alisema Makamba kwa simu leo.

Alisema kesho atazungumza na wanahabari namna utaratibu utakavyotumika wa kuviondoa viroba, baada ya waziri mkuu kutangaza.

Jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia wakazi wa Mji Mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro, alisema wamekaa na wenye viwanda na kukubaliana  wanaotengeza pombe hizo waziweke kwenye ukubwa unaokubalika.

Alisema agizo hilo linakwenda sambamba na vita dhidi ya dawa za kulevya, kwani mji wa Mirerani unaongoza kwa matumizi ya dawa hizo.