Kibatala ampa pole aliyekuwa DED B’moyo

Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema, Peter Kibatala.

Muktasari:

 “Tunasikitika nawe, na kukupa pole nyingi sana,” ameandika Kibatala jana katika ukurasa wake wa Facebook.

Dar es Salaam. Baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Azimina Mbilinyi kuenguliwa kwenye nafasi hiyo, Mkurugenzi wa Sheria wa Chadema, Peter Kibatala amempa pole.

 “Tunasikitika nawe, na kukupa pole nyingi sana,” ameandika Kibatala jana katika ukurasa wake wa Facebook.

Ikiwa pia, imepita siku moja baada ya kutoa ushahidi katika kesi za uchaguzi wilayani Kilombero kuhukumiwa  Kibatala ameongeza: “Tunakushukuru sana kwa kutoa ushahidi wa ukweli na wa haki katika kesi za uchaguzi majimbo ya Kilombero na Mlimba yaliyotolewa hukumu jana (Julai 29).”

Juzi, taarifa ya Ofisi ya Rais – Tamisemi iliyotolewa na Katibu Mkuu, Mussa Iyombe imeeleza kuwa Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mbilinyi kwa sababu hakuridhishwa na utendaji wake wa kazi.