Kigogo wa halmashauri aanza kurejesha fedha

Muktasari:

Fedha hizo anadaiwa kujikopesha kwa ajili ya kampeni za udiwani katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Mwanza. Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, Silvery Gregory ameanza kurejesha deni la Sh8.6 milioni anazodaiwa kujikopesha wakati akiwa mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ulemavu Tanzania (Chawata) mkoani Mwanza.

Fedha hizo anadaiwa kujikopesha kwa ajili ya kampeni za udiwani katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana.

Katibu wa muda wa Chawata mkoani Mwanza, Msafiri Makoba amesema Gregory amerejesha Sh200,000, kati ya Sh8.6 milioni anazodaiwa na chama hicho.

Hata hivyo, Gregory hakuwa tayari kuzungumza suala hilo akisema waulizwe Chawata.