Kilimanjaro wamwita Lukuvi akawatumbue mafisadi wa viwanja

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi.

Muktasari:

Kumekuwapo na madai kuwa viwanja vingi na nyumba viliuzwa kwa mamilioni ya shilingi, lakini wauzaji na wanunuzi waliandika mikataba inayoonyesha bei ya chini ili kukwepa kodi.

Moshi. Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro, wamemtaka Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kuchunguza mikataba ya mauziano ya nyumba na viwanja kuanzia miaka 10 iliyopita.

Kumekuwapo na madai kuwa viwanja vingi na nyumba viliuzwa kwa mamilioni ya shilingi, lakini wauzaji na wanunuzi waliandika mikataba inayoonyesha bei ya chini ili kukwepa kodi.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa tatizo kubwa lipo katika mji wa Moshi ambako mawakili wasio waaminifu wamekuwa wakiandika mikataba miwili ili kuikosesha Serikali mapato.