Kilio cha Watanzania ni Katiba- ACT

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelwa

Muktasari:

Kutokana na hali hiyo amemtaka Rais John Magufuli kuanza mchakato wa Katiba Mpya ili wananchi wawe na uwezo wa kuwawajibisha viongozi waliowachagua wanaposhindwa kutekeleza waliyoahidi.

Dar es Salaam. Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Msafiri Mtemelwa amesema kilio cha wananchi wengi ni katiba.

Kutokana na hali hiyo amemtaka Rais John Magufuli kuanza mchakato wa Katiba Mpya ili wananchi wawe na uwezo wa kuwawajibisha viongozi waliowachagua wanaposhindwa kutekeleza waliyoahidi.

“Katiba iliyopo haielezi wananchi kama wanaweza kumwajibisha mbunge wao, wabunge waliopitisha ndiyo walewale waliopitisha hii,” amesema Mtemelwa.

Ameiwataka viongozi wa dini kuunga mkono jitihada za kudai katiba mpya kutokana na sauti zao kusikilizwa na waumini na viongozi wakuu wa nchi.

Mtemelwa amesema chama hicho kitaanza utaratibu wa kuandika barua kwa Rais Magufuli ikiwa ni hatua za awali kutaka mabadiliko ya katiba.