Monday, January 28, 2013

Mwanamke mwenye hipsi kubwa duniani

 

LOS ANGELES, Marekani
WAKATI wanawake wengi duniani wakihangaika kukuza ukubwa wa makalio yao, huku wengine wakitumia njia ya kuvaa taiti zenye hipsi, wanaume wengi huko mjini Los Angeles wamejikuta  wakigeukageuka kumwangalia mwanamke mwenye makalio makubwa kupita kiasi kila apitapo njiani.

Mikel Ruffinelli ni mwanamke ambaye mpaka sasa ‘ameishavunja shingo’ za wanaume wengi. Makalio yake na hispi zake za asili zimemfanya atawazwe kuwa mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko wanawake wote duniani.

Mikel anayeishi nchini Marekani hajatumia dawa za mchina wala dawa zozote kama wafanyavyo akina dada wengine na ndiye aliyetambulishwa kuwa ndiye mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko wanawake duniani. Mpaka sasa mama huyo mwenye familia yake ana  hispi zenye  mita 2.44.

Umbile lake halikuja hivihivi, bali alikuwa ni mtu mwenye umbile la kawaida, licha ya kukiri kuwa ndugu zake wengi wana maumbile makubwa.

Hipsi za mwanamama huyo zimekuwa zikiongezeka siku baada ya siku kadiri alivyokuwa akijifungua watoto wake.

Mikel Ruffinelli, ambaye ni mama wa watoto wanne ana umri wa miaka 39 na ni mkazi wa Los Angeles amejisifia kuwa umbile lake limekuwa likiwachanganya wanaume wengi.
Akiwa na kiuno kidogo kisichoendana na mwili wake cha inchi 40, hispi zake zina mzunguko mkubwa wa inchi 96.
“Nalipenda umbile langu na sina mpango wa kujikondesha kwa diet,” alinena Mikel na kuongeza kuwa wanaume wengi wanapenda wanawake wenye maumbile makubwa siyo wale wembamba wembamba.”

Lakini kauli hiyo, imepingwa vikali na Jennifer Lopez, Kim Kardashian na Beyonce ambao wanasema inategemea na mwanaume husika na namna kile anachokipenda, lakini wakati mwingine hutegemea na mazoea ya mwanamume.

Mikel pamoja na kutamba na maumbile yake hayo ambayo anadai ni urithi toka kwenye familia yake ambapo karibuni ndugu zake wote wa kike nao wana hispi kubwa.

Mikel amelazimika kuishi tofauti ili aweze kuendana na umbile lake, hawezi kuenea kwenye gari ndogo hivyo gari analoliendesha ni kama lori.

Akiwa nyumbani kwake inabidi akae kwenye makochi yaliyotengenezwa kwa chuma badala ya mbao, pia kitanda chake nacho ni futi saba kwa saba.

Mume wa Mikel, Reggie Brooks mwenye umri wa miaka 40 ameelezea kupagawishwa na umbile la mkewe na ameongeza kuwa kila siku humsifia kwa kumwambia jinsi gani alivyo mrembo.

Mikel na mumewe wapo kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa na wamefanikiwa kupata watoto watatu ambapo mtoto wa kwanza wa Mikel alizaliwa katika ndoa yake ya kwanza kabla hajaachika na kuolewa na Reggie.

Mikel ameongeza kuwa kwa miaka mitano iliyopita amekuwa akijiingizia kipato chake kwa kupiga picha za mavazi kwa ajili ya Tovuti ya Big Beautiful Women ambapo katika kila wakati anapoitwa kupigwa picha hulipwa Dola 1,000.

Anasema, “Mara nyingi ninapokuwa katika picha za tovuti, ninajitahidi sana kuchagua nguo zitazonifaa. Hivyo wabunifu wananifunza kuuelewa mwili wangu na nguo ipi inaufaa, nami sina tatizo katika suala la uvaaji.”

Mikel Ruffinelli, mwenye uzito wa kilogramu 191 amekuwa na unene uliozidi tofauti na urefu alionao.

“Ninaipenda shepu yangu na sina matatizo ya kiafya hivyo sioni sababu ya kupunguza mwili kwa kujinyima kula na wakati huu nina mpango wa kuongeza mlo ikiwezekana,” anasema Mikel ambaye hula kuku mzima na vyakula vingine vya wanga na protini kwa siku.

Mazoezi ya Mikel hutegemea na siku husika, mara nyingi anasema hufanya matembezi ya jioni akiwa na mume wake na wakati mwingine huamua kutembea sehemu moja hadi nyingine kuzunguka nyumba yake.

Mume wake ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kompyuta anasema anavutiwa zaidi na mkewe na hapendi kabisa apungue mwili na anadhani ni mwili mzuri tu kwa kuwa hajatumia madawa kuukuza.

Alipokuwa na umri wa miaka 22, Mikel alipata mtoto wake wa kwanza Andrew ambaye hivi sasa ana miaka 19, kutoka katika uhusiano uliopita na hapo ndipo alipoanza kuongezeka uzito.
Alianza kwa kuongezeka kilo 82.5 na baadaye alifikia kilo 108. Baadaye alikutana na Reggie na baada ya miongo mitatu sasa wana watoto watatu. Destynee, 13, Autumn, nane na Justyce, saba. Na hivi sasa hipsi zake zimetanuka mpaka kufikia uzito wa kilogramu 191.

“Nilikuwa nikiongezeka nikiwa na ujauzito.  Sikujua ni kwa nini uzito uliongezeka sana na hipsi kuwa kubwa, niliendelea kula zaidi, lakini nilivyojifungua sikuweza kurudia mwili wangu wa awali, hivyo ndivyo ilivyokuwa.”

Mikel, ambaye alisomea Shahada ya Saikolojia, ni mwenye afya na hamu kubwa ya kula na anayeweza kumaliza chakula kingi kwa siku.

“Ni maajabu kuona mwanamke anakula kalori 3000 kwa siku lakini kwangu mimi ni jambo la kawaida.

“Ninapata kifungua kinywa cha mayai mawili, soseji na viazi kadhaa. Mchana chakula changu kikubwa ni samaki wa kukaanga na chakula cha wanga kingi tu, lakini chakula cha jioni huwa ninahitaji zaidi mlo mzito.

“Ninapenda kutengeneza kuku wa kuoka wawili wakubwa na wali. Nina fungu kubwa, lakini ninapenda chakula kizuri, ninaandaa pia vitafunwa kama karanga, klipsi na vingine vinavyoweza kuliwa usiku.”

Kama ilivyo kwa mwili wake, Mikel anasema anaamini pia vyakula hivyo humsaidia kuulinda mwili wake na anazidi kukua akiwa salama kwa shepu na saizi ya mwili wake.

“Mwanzoni nilijitahidi sana kuwa makini na umbile langu na niliweza kupunguza hipsi kwa kunywa maziwa sana, lakini haikufanya kazi. Na kwa sasa ninazidi kuwa mtu mzima, nimejifunza kuupenda mwili wangu na sasa sina hofu tena kuonyesha mwili wangu na kujivunia.”

Mikel pia anafanya jitihada za kuwa na afya, huku akijitahidi kucheki afya yake mara kwa mara ili asikumbane na magonjwa ya moyo na mengineyo kama hayo.

Kwa miaka mingi Mikel amekua akikumbana na makwazo mbalimbali kutoka kwa watu wanaomzunguka, na sana sana ni kwa wale ambao hawakuwahi kumtia machoni, lakini amejifunza kuwapuuza.

“Sitaki kuwa mwili mkubwa zaidi ya hapa, lakini sihitaji kupoteza uzito wangu wa mwili. Nadhani nahamasisha wanawake kufikiri “Kuwa na furaha na mwili wake na hivi ndivyo  nifanyavyo mimi!.”
Imeandaliwa na Harieth Makweta kwa msaada wa mtandao

-->