Hofu ya bomu yaikumba CNN

Muktasari:

  • Kisa hicho kilichodumu kwa dakika 90 kilikumbusha tukio jingine kama hilo Oktoba mwaka huu baada ya kilipuzi kugundulika katika ofisi za makao makuu ya CNN, New York.

New York, Marekani. Hofu ya kutokea shambulio la bomu katika ofisi za mtandao wa habari wa CNN mjini hapa Alhamisi zilisababisha wafanyakazi kuondolewa kwa ajili ya usalama lakini hakuna kilipuzi kilichokutwa na polisi walisema hali shwari.
Kisa hicho kilichodumu kwa dakika 90 kilikumbusha tukio jingine kama hilo Oktoba mwaka huu baada ya kilipuzi kugundulika katika ofisi za makao makuu ya CNN, New York.
Kengele za kuashiria moto zililia ndani ya chumba cha ikiwa ni ishara ya watu kuondolewa muda mfupi baada ya saa 4:30 usiku, shirika la CNN lilisema katika tovuti yake. Saa moja baadaye shirika hilo lilikuwa likitangaza kupitia Skype.