China yapitisha sheria ya uzazi

Muktasari:

  • Sheria tata, ambazo zilikuwa zikiwabana wanandoa wengi wa mijini kuzaa mtoto mmoja na vijijini kuzaa wawili tu, zilianzishwa miaka ya 1970 katika juhudi za taifa hili kubwa kudhibiti ongezeko la watu waweze kuendana na raslimali zilizopo.

Beijing, China. Serikali inafikiria kufuta sera ya sasa inayowabana wazazi kuzaa mtoto mmoja, ofisa mmoja katika ofisi ya uzazi wa mpango amesema akitaja sababu kuwa kukabiliana na ongezeko la wazee katika jamii na pengo la kijinsia.

Sheria tata, ambazo zilikuwa zikiwabana wanandoa wengi wa mijini kuzaa mtoto mmoja na vijijini kuzaa wawili tu, zilianzishwa miaka ya 1970 katika juhudi za taifa hili kubwa kudhibiti ongezeko la watu waweze kuendana na raslimali zilizopo.

Lakini sasa naibu waziri katika Tume ya Taifa ya Idadi ya Watu na Mpango wa Uzazi Zhao Baige alisema maofisa wanapitia maelezo ya kina kuhusu athari za kimazingira, kijamii na nyinginezo katika kubadili sheria.

Alipoulizwa ikiwa wana mpango wa kufuta sera ya kuzaa mtoto mmoja Baige aliwaambia wanahabari jijini Beijing kwamba kuna “mchakato mkali” wa kiutafiti hivi sasa.

Sababu za kupitia upya

Baraza la Taifa, ambalo ni Baraza la Mawaziri limeamuru ufanyike utafiti kuhusu madhara ya kuondoa sera hiyo iliyodumu karibu miongo minne ikitaka kuweka mabadiliko ya kitaifa, walisema watu walioomba wasitajwe majina wakati serikali inafanya majadiliano ili iweze kufikia uamuzi.

Uongozi unataka kupunguza pengo la wazee na kuondoa chanzo hicho kikubwa cha ukosoaji wa kimataifa, mtu mmoja alisema.

Mtu huyo alisema mapendekezo yanayojadiliwa kwa sasa yatakuwa mbadala wa sera ya kudhibiti idadi ya watu ambapo mmoja ameita kuwa ni “uhuru wa uzazi” kuwaruhusa watu kuamua idadi ya watoto wa kuzaa.

Mtu mwingine alisema uamuzi huo unaweza kutolewa mapema iwezekano robo ya nne yam waka naakaongeza inawezekanao tangazo rasmi linaweza kusogezwa hadi mwaka 2019.