DJ Rajoelina aongoza matokeo Madagascar

Muktasari:

  • Baada ya matokeo kutoka asilimia 30.6 ya vituo vya kupigia kura, Rajoelina alijikusanyia asilimia 40.9 akifuatiwa kwa karibu na Ravalomanana aliyepata asilimia 36, Tume ya Uchaguzi, CENI, ilisema Jumapili.

Antananarivo, Madagascar. Matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu wa Madagascar uliofanyika wiki iliyopita yanaonyesha kwamba rais wa zamani Andry Rajoelina anaongoza akifuatiwa na mpinzani wake Marc Ravalomanana.
Rajoelina aliyechukuliwa kuwa ni DJ na Ravalomanana, kwa matokeo ya awali ya uchaguzi wa Novemba 7 katika kisiwa hicho ambacho hakijawa na utulivu wa kisiasa tangu kilipopata uhuru kutoka Ufaransa mwaka 1960, walikuwa mbele ya wengine 34.
Baada ya matokeo kutoka asilimia 30.6 ya vituo vya kupigia kura, Rajoelina alijikusanyia asilimia 40.9 akifuatiwa kwa karibu na Ravalomanana aliyepata asilimia 36, Tume ya uchaguzi, CENI, ilisema Jumapili.
Kambi ya Ravalomanana ilipanga kutembelea ofisi za CENI Jumatatu asubuhi kuhoji matokeo yalivyoendelea kushuka kwa upande wao.