EU yapeleka vikosi kuzima moto Ugiriki

Muktasari:

Umoja wa Ulaya (EU) ulipeleka vikosi vya zima moto nchini Ugiriki humo huku Hispania ikijipanga kupeleka ndege mbili za kumwaga maji.

Athens,Ugiriki. Baada ya moto mkubwa kuteketeza msitu na magari kadhaa huku zaidi ya watu 70 wakipoteza maisha  maeneo ya mji na vijiji karibu na mji mkuu Athens, Serikali imetangaza maombolezo ya kitaifa.

Umoja wa Ulaya (EU) ulipeleka vikosi vya zima moto nchini Ugiriki humo huku Hispania ikijipanga kupeleka ndege mbili za kumwaga maji.

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Jean-Claude Juncker amesema kila kitu kitafanyika kutoa msaada katika muda wote unaohitajika.

Nchi za Umoja wa Ulaya za Uhispania, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Ureno, Lithuania, Denmark, Poland na Austria pia zimeitikia wito huo.

 

Mpaka sasa zaidi ya  miili 26 iligunduliwa kwa pamoja ikiwa juu ya mwamba pembezoni mwa bahari katika eneo la Mati, moja kati ya miji iliyoathirika zaidi.

Baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamesema walilazimika kukimbilia baharini kujiokoa walipoona wamezingirwa na moto huo.

 

Hata hivyo, Serikali ina shaka kuhusiana na chanzo cha moto huo na kwamba huenda uliwashwa  kwa makusudi na watu wasiojulikana.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alex Tsipras (Kwa masikitiko) alisema janga hilo limeathiri nchi nzima.

''Nchi inapitia katika wakati mgumu sana. Mamia ya watu wamefariki na hili linamuumiza kila mmoja haswa kwa familia zilizopoteza wapendwa wao. Leo (jana) Ugiriki inaomboleza, na kwa kumbukumbu ya wale wote waliofariki tunatangaza siku tatu za maombolezo.''

Amesema Tsipras Theofilaktos Logothetis  mmoja wa waathirika alisema alikua mmoja wa wale waliokua wa mwisho kabisa kutoka nyumbani kabla ya miale ya moto kufika kwa majirani zake.

Moto ni kama ulikuwa unatukimbiza, aliyekuwa anaweza kuondoka kabla haujafika ilikua bahati. Mtu aliyekuwa kulia kwangu nilipokuwa nikiendesha kuelekea barabara kuu aliunguzwa mpaka akawa mkaa.''

Serikali ya Ugiriki inasema kuna uwezekano mkubwa watu wengi zaidi wakawa wamefariki katika tukio hilo ambalo limeacha simanzi kwa nchi nzima.