Familia yalilia fidia ya Kenneth Matiba

Muktasari:

  • Hayo yalielezwa na aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini Wanyiri Kihoro ambaye ni ndugu wa karibu na Matiba akidai kwamba amesikitishwa na uwepo wa deni hilo licha ya mahakama kuamuru marehemu alipwe fidia yake.

Nairobi, Kenya. Serikali ilikuwa haijamlipa fidia ya Sh945milioni mwanasiasa mkongwe, Kenneth Matiba aliyefariki dunia nchini Kenya Jumapili.

Hayo yalielezwa na aliyekuwa Mbunge wa Nyeri Mjini Wanyiri Kihoro ambaye ni ndugu wa karibu na Matiba akidai kwamba amesikitishwa na uwepo wa deni hilo licha ya mahakama kuamuru marehemu alipwe fidia yake.

Marehemu alipewa fidia hiyo kwa kuzuiliwa na kuteswa kizuizini alipokamatwa kwa kupigania kurejelewa kwa mfumo wa utawala wa vyama vingi mapema miaka ya 1990

“Inasikitisha kuwa Mzee Matiba amefariki kabla ya Serikali kumlipa fidia ilhali mahakama ilitoa uamuzi huo miezi tisa iliyopita,’’ alisema Kihoro alipokuwa anahojiwa na Citizen TV.

Alisema mahakama imetoa uamuzi wake miaka tisa iliyopita lakini Serikali imeshindwa kumlipa licha ya kwamba alikuwa mgonjwa.