Kenyatta amwondoa Ruto kwenye Twitter

Muktasari:

  • Kutokana na uamuzi huo rais sasa hawezi kusoma ujumbe wowote wa kwenye Twitter wa naibu wake huyo katika akaunti yake. Hadi mwishoni mwa wiki, Kenyatta bado alikuwa mmoja wa wafuasi wake.

Nairobi, Kenya. Rais Uhuru Kenyatta ameondoa jina la makamu wake William Ruto kati ya washirika wake kwenye Twitter, hatua iliyoanza kuzua mjadala kwenye mitandao ya kijamii.
Kutokana na uamuzi huo rais sasa hawezi kusoma ujumbe wowote wa kwenye Twitter wa naibu wake huyo katika akaunti yake. Hadi mwishoni mwa wiki, Kenyatta bado alikuwa mmoja wa wafuasi wake.
Japokuwa hatua hii haina thamani yoyote kwa usoni, matumizi ya mitandao ya kijamii yanaonyesha tabia za watu hivyo suala hilo haliwezi kupuuzwa.
Kenyatta alianza kupunguza wafuasi wake tangu Aprili 2016, alipowaondoa watu 600 hadi akabaki na watu 11. Aliwaondoa viongozi wengi wa kimataifa, magavana na mawaziri.
Miongoni mwa hao 11 aliokuwa anaendelea kusoma habari wanazotuma kwa njia ya Twitter walikuwa naibu wake, mkewe Margaret Kenyatta na msemaji wa Ikulu Manoah Esipisu.
Jicho la mwanahabari wa Daily Nation Augustine Sang ambaye ni mtumiaji mkubwa wa mitandao ya kijamii ndilo lililobaini.
Katika siku za hivi karibuni imeelezwa kuna mvutano ndani ya Jubilee tangu Kenyatta aliposhikana mkono na kiongozi mkuu wa upinzani na aliyewahi kuwa waziri mkuu Raila Odinga.