Kim asimamia majaribio silaha mpya

Muktasari:

  • Hakuna habari za kina kuhusu silaha hiyo au kama ni mpya, lakini majaribio hayo ni ishara ya hivi karibuni kuwa Korea Kaskazini imejiandaa kurejea katika uhusiano wa mapambano zaidi dhidi ya Marekani ikiwa mazungumzo baina yao yatazidi kuzorota.




Seoul, Korea Kusini. Korea Kaskazini imefanyia majaribio silaha “mpya iliyoboreshwa kuwa ya kisasa” zaidi katika tukio lililosimamiwa na kiongozi wa nchi Kim Jong Un, vyombo vya habari vimeripoti Ijumaa katikati ya mazungumzo yanayolegalega kuhusu ukomeshwaji silaha za nyuklia na Marekani.
Hakuna habari za kina kuhusu silaha hiyo au kama ni mpya, lakini majaribio hayo ni ishara ya hivi karibuni kuwa Korea Kaskazini imejiandaa kurejea katika uhusiano wa mapambano zaidi dhidi ya Marekani ikiwa mazungumzo baina yao yatazidi kuzorota.
"Amechuchumalia kimapambano zaidi mazungumzo na Marekani na anaashiria kwamba amejiandaa kutosalimu na anaweza tu kurudi kwenye utaratibu wa zamani ikiwa (Marekani) haibadili mtazamo wake," Josh Pollack, mtafiti mshirika katika Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa Middlebury ya Monterrey, aliiambia CNN.