Mpinzani mkuu Iraq aongoza katika matokeo

Muktasari:

  • Hadi nusu ya matokeo yakiwa yamehesabiwa na kutangazwa, kambi inayoongozwa na aliyekuwa kamanda wa vikosi vya angani na inayoungwa mkono na Iran ya Hadi al-Amiri ilishika nafasi ya pili huku waziri mkuu Haider al-Abadi akiangukia nafasi ya tatu.

Baghdad, Iraq. Kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa madhehebu ya Shia Muqtada al-Sadr, hadi kufikia mchana jana alikuwa akiongoza katika matokeo ya uchaguzi wa wabunge uliofanyika Jumapili.
Hadi nusu ya matokeo yakiwa yamehesabiwa na kutangazwa, kambi inayoongozwa na aliyekuwa kamanda wa vikosi vya angani na inayoungwa mkono na Iran ya Hadi al-Amiri ilishika nafasi ya pili huku waziri mkuu Haider al-Abadi akiangukia nafasi ya tatu.
Matokeo yote yalitarajiwa kutangazwa jana jioni baada ya kukamilisha kupokea na kuhesabu kura kutoka majimbo manane likiwemo la Nineveh ambalo ni la pili kuwa na viti vingi bungeni baada ya Baghdad.
Uchaguzi huo wa wabunge unatumika kama kura ya maoni tangu lilipoangushwa kundi la dola ya Kiislamu la ISIS mwaka 2017.