EU walivalia njuga suala la Syria

Muktasari:

  • Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema  kwamba mashambulizi yaliyofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa kuwa ni muhimu na sahihi, lakini mataifa mengine wanachama wa Umoja huo wanapinga hatua hiyo.

Mawaziri wa Mambo ya Nje  wa Umoja wa Ulaya(EU) wanajaribu kuwa  na msimamo mmoja katika mazungumzo mjini Luxembourg leo Aprili 16  licha ya tofauti zilizopo kuhusiana na mashambulizi dhidi ya Syria.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema  kwamba mashambulizi yaliyofanywa na Marekani, Uingereza na Ufaransa kuwa ni muhimu na sahihi, lakini mataifa mengine wanachama wa Umoja huo wanapinga hatua hiyo.

Wakati mataifa 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wakikubaliana kwamba shambulio la gesi ya sumu ni kitendo ambacho hakiwezi kuachwa bila ya kuadhibiwa, taarifa zilizotolewa na mkuu wa sera za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini Jumamosi hazikufikia kuidhinisha mashambulizi, akisema  wale wanaohusika, watawajibishwa kwa kukiuka sheria za kimataifa.