Swahiba mwingine wa Grace Mugabe mbaroni

Muktasari:

  • Katika kipindi kirefu waziri huyo alikuwa Afrika Kusini alikokimbilia baada ya kusikia kuwa anatafutwa na polisi lakini alilazimika kurejea baada ya kusikia anasakwa na polisi wa kimataifa - Interpol

Harare, Zimbabwe. Waziri wa zamani Saviour Kasukuwere ametiwa mbaroni na kukamatwa kwake kulifanikishwa baada ya polisi Zimbabwe kuomba msaada wa jeshi la kimataifa Interpol, Mahakama ya Hakimu Mkazi Harare iliambiwa Jumanne.
Kasukuwere ambaye alikuwa Waziri wa Serikali za Mitaa enzi za Rais Robert Mugabe, alitiwa mbaroni Jumatatu na akafikishwa mahakamani Jumanne ambako anashtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka yanayohusiana na ukiukwaji wa mchakato wa zabuni badala yake ekari kadhaa za ardhi ya Serikali alipewa dada wa Grace Mugabe.
Hata hivyo, baadaye aliachiwa na Hakimu Hosiah Mujaya anayesikiliza kesi hiyo kwa dhamana ya dola 3,000 pamoja na masharti kadhaa.