Waliowaudhi Trump, Melania matatani

Muktasari:

  • Katika hotuba iliyotolewa hadharani ikiibuka kutoka kusikojulikana, ofisi ya mke wa rais ilionya kwamba naibu mshauri wa usalama wa taifa Mira Ricardel, ambaye inaripotiwa alikorofishana naye katika safari ya hivi karibuni barani Afrika “kamwe hastahili heshima ya kuhudumu katika Ikulu ya White House."

Washington, Marekani. Hali ilivyo, katika Ikulu ya White House, hakuna mtumishi yeyote anayejua ni lini shoka litamwangukia shingoni au kukumbwa na kizaazaa hadi kuondolewa.
Katika kipindi kilichojaa hasira na ghadhabu kikiishia kuonyesha mamlaka aliyonayo mke wa Rais Donald Trump, Melania Trump, hali ilizidi kuwa mbaya katika historia ya utawala unaodaiwa kushindwa kazi Jumanne na kuwaacha maofisa wakiwa hawajui na wamechanganyikiwa.  
Hata ikilinganishwa na namna maofisa wa juu walivyotibuana, mzozo wa urasimu na vurugu ambazo huonekana jambo la kawaida katika Ikulu ya White House ya Trump, hatua ya ghafla ya Melania dhidi ya ofisa wa sera za kigeni lilikuwa sawa na shambulio la bomu.
Katika hotuba iliyotolewa hadharani ikiibuka kutoka kusikojulikana, ofisi ya mke wa rais ilionya kwamba naibu mshauri wa usalama wa taifa Mira Ricardel, ambaye inaripotiwa alikorofishana naye katika safari ya hivi karibuni barani Afrika “kamwe hastahili heshima ya kuhudumu katika Ikulu ya White House."
Haya yanakuja baada ya kufahamika kwamba Rais Trump anatarajia kumfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani, Kirstjen Nielsen na anafikiria kumpumzisha mnadhimu mkuu John Kelly katika juhudi za kupanga na kupangua upya safu yake.
Trump amekuwa akifikiria kitambo kumwondoa Nielsen, mtu anayekingiwa kifua na Kelly ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na baadaye kuwa mnadhimu wa Ikulu ya White House.