Wasichana 239,000 hufa kila mwaka India kwa kubaguliwa

Muktasari:

Ubaguzi wa kijinsia wanaofanyiwa watoto wa kike hauwi tu kuzuia wasizaliwe bali unaweza kuharakisha kifo kwa waliozaliwa,” alisema mhariri mwenza wa utafiti huo Christophe Guilmoto wa Chuo Kikuu cha Paris Descartes.

New Delhi, India. Wastani wa watoto wa kike wapatao 239,000 wenye umri chini ya miaka mitano hufariki dunia nchini kila mwaka kutokana na wazazi wengi kupendelea watoto wa kiume dhidi ya wasichana.
Wanasayansi waliofanya utafiti huo na matokeo yake kuchapishwa Jumanne katika jarida la The Lancet walibaini uwiano mgumu kati ya wanaume na wanawake, na kwamba zaidi ya wanawake milioni 63 “kitakwimu wamepotea” kote nchini sababu inaweza kuwa matokeo idadi kubwa ya vifo vya wanawake, utafiti wa kiuchumi wa serikali umeonyesha.
Moja ya sababu zilizozoeleka zilizotajwa kuwa kiini cha idadi ya vifo vingi vya wanawake nchini India ni utoaji mimba wa kuchagua watoto, lakini uchunguzi ulibaini “ubaguzi wanaofanyiwa watoto wa kike," jambo linaloonyesha tatizo si kabla ya kuzaliwa kwao bali huendelea hata wakishazaliwa.
"Ubaguzi wa kijinsia wanaofanyiwa watoto wa kike hauwi tu kuzuia wasizaliwe bali unaweza kuharakisha kifo kwa waliozaliwa,” alisema mhariri mwenza wa utafiti huo Christophe Guilmoto wa Chuo Kikuu cha Paris Descartes.
"Usawa wa kijinsia hauhusu tu haki za elimu, ajira au uwakilishi kisiasa; bali pia unahusu matunzo, chanjo, na lishe kwa wasichana na hatimaye kuishi kwao,” alisema Guilmoto.
Utafiti huo umebaini kwamba maeneo ya vijijini ambako kuna watu wengi wanaokosa matunzo mazuri ni wasichana. Majimbo makubwa ya Kaskazini mwa India - Uttar Pradesh, Bihar, Rajasthan, na Madhya Pradesh – takwimu zinaonyesha ndiyo yana theluthi mbili ya vifo vya wanawake nchini India.