Kishindo mahakamani, tajiri afikisha mashtaka 400 Dar

Mfanyabiashara Mohammed Mustafa Yusufali .

Muktasari:

  • Jana, Yusufali na mfanyabiashara maarufu jijini Arusha Samweli Lema walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa  mashitaka 222, ingawa baadhi ni mashitaka yanayomkabili Lema tu.
  • Hivi karibuni, Yusufali alishtakiwa pamoja na wenzake wanne kwa makosa 199 ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh15.6 bilioni.

Dar es Salaam. Mfanyabiashara Mohammed Mustafa Yusufali amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka 222 na kufanya akabiliwe na mashtaka yanayokaribia 400.

Jana, Yusufali na mfanyabiashara maarufu jijini Arusha Samweli Lema walipandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa  mashitaka 222, ingawa baadhi ni mashitaka yanayomkabili Lema tu.

 Hivi karibuni, Yusufali alishtakiwa pamoja na wenzake wanne kwa makosa 199 ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh15.6 bilioni.

Lema na Yusufali wanakabiliwa na kesi hiyo ya uhujumu uchumi, ambayo inahusisha pia mashtaka ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh14.05 bilioni na utakatishaji Fedha.

Lema, ambaye anamiliki kampuni mbalimbali ikiwamo ya Northern Engineering Works Limited na Elerai Constructions Ltd, na Yusufali walisomewa mashtaka hayo jana kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Yusufali na wenzake wanne wanakabiliwa na mashtaka mengine 199 ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia zisizo halali na kuwasilisha nyaraka za kughushi, walifikishwa mahakamani siku chache baada ya Rais John Magufuli kusema hadharani kuwa kuna mtu anajipatia Sh7 milioni kwa kila dakika.