Kisiwa cha Latham chaibua mjadala Zanzibar

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman

Dar/ Zanzibar. Wakati Serikali ikisema mzozo wa umiliki wa Kisiwa cha Latham kati ya Tanganyika na Zanzibar ulishatatuliwa, mhadhara kuhusu suala hilo unaendelea, na leo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Othman Masoud Othman atawasilisha mada kuhusu suala hilo.

Othman atawasilisha mada hiyo kwenye ofisi za Taasisi ya Utafiti wa Sera za Umma ya Zanzibar (ZIRPP) zilizoko nyuma ya jengo la Majestic kisiwani Unguja.

Umiliki wa kisiwa hicho umekuwa na utata tangu 1898 wakati Zanzibar ikiwa chini ya utawala wa Sultan wa Oman na Tanganyika (Tanzania Bara) ikitawaliwa na Mjerumani.