Jinsi Mbunge Mtolea alivyolamba matapishi yake

Muktasari:

Kujiuzulu kwa mbunge huyo kumekuwa ni kinyume na msimamo wake wa awali aliowahi kuutoa.

Dar/ Dodoma. Mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea leo Alhamisi Novemba 15, 2018 ameutangazia umma kutokea bungeni jijini Dodoma kuwa amejiuzulu ubunge na nyadhifa zake zote kwenye chama chake.

Kujiuzulu kwa mbunge huyo kumekuwa ni kinyume na msimamo wake wa awali aliowahi kuutoa.

Mtolea aliwahi kuwakosoa wabunge wenzake wa upinzani waliojivua ubunge na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), akisema wanaisababishia Serikali hasara.

Alitoa kauli hiyo Desemba 8, 2017 siku ya Ijumaa akiwa ameambatana na Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa, kwenye mahojiano maalum na kipindi cha Morning Trumpet kinachorushwa na Televisheni ya Azam.

Katika mahojiano hayo, alipoulizwa kuhusu wimbi la wanasiasa wanaohama vyama vya siasa, Mtolea aliwakosoa wanasiasa hao na kusema wanaisababishia Serikali hasara.

“Hawa wanaosema wamefurahishwa na kazi ya Rais, hivi kumuunga mkono Rais ndio umtie hasara, kwa sababu ukijivua ubunge, jimbo lile unaliacha wazi na uchaguzi lazima ufanywe kwa matakwa ya sheria, leo kurudia uchaguzi kwa jimbo moja ni takriban Sh70bilioni, sasa Je unamsaidiaje Rais kwa kuitia hasara Serikali kwa kurudia uchaguzi kwa gharama hizo.” Alisema Mtolea.

Aidha, Mtolea katika kipindi hicho cha Morning Trumpet, pia alikosoa madai ya wanasiasa waliohama vyama vyao na kuhamia CCM wakidai vyama vya upinzani vimeishiwa ajenda.

“Wasichokifahamu ni kwamba vyama vya siasa haviendeshwi kwa ajenda bali vinaendeshwa kwa itikadi au misingi iliyosababisha kuundwa kwa chama cha siasa ili waweze kumaliza kero mbalimbali nchini na njia ya haraka ya kufikia maendeleo ya nchi,” alisema Mtolea.

Hata hivyo, leo bungeni, Mtolea akitangaza kujiuzulu amesema sababu ya kujiuzulu nafasi zake hizo ni mgogoro wa wanachama wanaomuunga mkono mwenyekiti wa Taifa



Katika mahojiano hayo, alipoulizwa kuhusu wimbi la wanasiasa wanaohama vyama vya siasa, Mtolea aliwakosoa wanasiasa hao na kusema wanaisababishia serikali hasara.

“Hawa wanaosema wamefurahishwa na kazi ya Rais, hivi kumuunga mkono Rais ndio umtie hasara, kwa sababu ukijivua ubunge, jimbo lile unaliacha wazi na uchaguzi lazima ufanywe kwa matakwa ya sheria, leo kurudia uchaguzi kwa jimbo moja ni takriban Sh70bilioni, sasa Je unamsaidiaje Rais kwa kuitia hasara Serikali kwa kurudia uchaguzi kwa gharama hizo.” Alisema Mtolea

Aidha, Mtolea katika kipindi hicho cha Morning Trumpet, pia alikosoa madai ya wanasiasa waliohama vyama vyao na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) wakidai vyama vya upinzani vimeishiwa ajenda.

“Wasichokifahamu ni kwamba vyama vya siasa haviendeshwi kwa ajenda bali vinaendeshwa kwa itikadi au misingi iliyosababisha kuundwa kwa chama cha siasa ili waweze kumaliza kero mbalimbali nchini na njia ya haraka ya kufikia maendeleo ya nchi,” alisema Mtolea.