Aliyejirekodi video za ngono na Wema Sepetu asakwa na polisi

Muktasari:

Leo Jumanne Novemba 6, 2018, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema litamfikisha mahakamani mwanaume aliyeonekana katika picha za mapenzi na msanii Wema Sepetu


Dar es Salaam. Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wamesema wanamsaka mwanaume aliyeonekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa na msanii Wema Sepetu.

Akizungumza leo Jumanne Novemba 6, 2018, Kaimu Kamanda wa Kanda hiyo,  Liberatus Sabas amesema polisi wanaendelea kumsaka mwanaume huyo na wakimpata wanamfikisha mahakamani.

“Polisi tunaendelea kumtafuta huyu jamaa, hatujakata tamaa na ikiwa tutamkamata lazima tumfikishe mahakamani kwani ana kesi ya kujibu,’’ amesema.

Amesema kwamba watu wanadhani labda jeshi la polisi limeshaachana na mwanaume huyo lakini bado ni mtuhumiwa na hivyo akikamatwa anapelekwa mahakamani.

Soma zaidi: