Buju Banton aachiwa huru baada ya kukaa jela miaka saba

Muktasari:

Alipatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya


Msanii maarufu wa muziki wa reggae duniani, Buju Banton hatimaye ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka nane nchini Marekani.

Buju ambaye jina lake halisi ni Mark Myre alikamatwa Disemba 2009 akishukiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Ilidaiwa kuwa  Buju Bunton alijaribu kufanya biashara ya dawa za kulevya kwa kuingiza kilo tano za cocaine nchini Marekani akitokea Hispania.

Baada ya kusomewa shtaka  hilo Februari 2011, msanii huyo wa muziki wa Reggae alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.

Hukumu ya kifungo chake ilipaswa kuisha Februari 2019, lakini baadaye ilibadilishwa kuwa Disemba 8, 2018.

“ Nataka kuwashirikisha habari njema na nguvu ya muziki wangu, nataka kuendelea kutengeneza muziki ambao nimejitoa katika maisha yangu, natazamia kuipata fursa ya kuwashukuru mashabiki wangu na kila mmoja aliyeniunga mkono”, alisema Buju Banton.

Waziri wa Usalama nchini Jamaica, Horace Chang anasema msanii huyo hawezi kupewa mapokezi ya heshima kwa sababu alipatakana na hatia ya kujihusisha na dawa za kulevya lakini hiyo haifuti ukweli kwamba ni msanii mkubwa anayeheshimika.

Buju Bunton ni msanii mkubwa nchini humo akimfuatia Bob Marley ambaye katika kipindi cha miaka 30 amevunja rekodi za mauzo na kujaza kumbi za burudani duniani.