Diamond Platnumz, Rayvanny wafungiwa kwa muda usiojulikana

Muktasari:

  • Tamasha la Wasafi nalo lafutiwa kibali chake

Baraza la Sanaa nchini (Basata) limewafungia  wanamuziki  Diamond Platnumz na Rayvanny  kutojihusisha shughuli za sanaa kwa muda usiojulikana.
Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa leo Desemba 18, imesema limefikia uamuzi huo baada ya wasanii hao kuonyesha dharau kwa mamlaka zinazosimamia shughuli za sanaa nchini, kwa kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.
Mbali na kuwafungia wanamuziki hao, Baraza limetangaza kukifuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival linaloendelea nchini.
Wimbo wa Mwanza ambao uliowaingiza matatani ulifungiwa Novemba 12.
Juzi, Basata iliahidi kutoa taarifa rasmi baada ya wasanii hao kuonekana jukwaani katika Tamasha la Wasafi jijini Mwanza wakitumbuiza wimbo huo.