Jaji wa Vioja Mahakamani auawa

Muktasari:

  • Mwigizaji huyo alibebwa na kukimbizwa haraka katika Hospitali ya Shalom kwa matibabu ya dharura na huko ndiko ilitangazwa kwamba amefariki dunia alipofikishwa.
  • Ripoti ya polisi ilisema, "Iliripotiwa kwamba Jamal Nassul Gaddafi (39), alikuwa kwenye sherehe katika Hoteli ya Arks karibu na Hoteli ya 67 Airport usiku wa Desemba 11, 2018. Uliibuka mzozo kati yake na rafiki yake Grace Kanamu Namu (40). Alichukua kisu na kumchoma."
  • Kabla ya kuzuka mkasa huo mbaya, wawili hao walikuwa majirani eneo la Syokimau. Wote wawili walikuwa wametalikiwa na hivyo waliamua kuanza maisha pamoja.

Nairobi, Kenya. Jamal Nassul Rashid ambaye huigiza kama jaji katika mfululizo wa vipindi vya Vioja Mahakamani vinavyorushwa kupitia Televisheni ya KBC aliuawa Jumanne kwa kuchomwa kisu baada ya kuzuka mzozo.
Habari zinasema, Jamal alichomwa kisu na rafiki yake wa kike aitwaye Grace Kanamu Namu, 40, kwa kutumia kisu cha jikoni katika Hoteli ya Arks majira ya saa 12:15 jioni.
Mwigizaji huyo alibebwa na kukimbizwa haraka katika Hospitali ya Shalom kwa matibabu ya dharura na huko ndiko ilitangazwa kwamba amefariki dunia alipofikishwa.
Ripoti ya polisi ilisema, "Iliripotiwa kwamba Jamal Nassul Gaddafi (39), alikuwa kwenye sherehe katika Hoteli ya Arks karibu na Hoteli ya 67 Airport usiku wa Desemba 11, 2018. Uliibuka mzozo kati yake na rafiki yake Grace Kanamu Namu (40). Alichukua kisu na kumchoma."
Kabla ya kuzuka mkasa huo mbaya, wawili hao walikuwa majirani eneo la Syokimau. Wote wawili walikuwa wametalikiwa na hivyo waliamua kuanza maisha pamoja.
Jamal pia alishiriki kama Baba Junior katika mfululizo wa vipindi viitwavyo Junior katika Televisheni ya KTN.